Bosi wa TRC amjibu Kigwangalla



Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amekanusha madai ya Mbunge wa Nzega Vijijini, Dk Hamisi Kigwangalla kuwa mabehewa ya treni ya kisasa yaliyoletwa nchini ni mtumba.

Novemba 25 TRC ilipokea mabehewa 14 kati ya 59 ya masafa marefu, huku pia ikitarajia kupata vichwa 10 vya treni ya umeme (EMU).

Akizungumza jana jijini Dodoma baada ya kufanya safari ya majaribio ya treni kutoka Dar es Salaam wakiwa na wenyeviti wa CCM, Kadogosa amesema, mabehewa yaliyoletwa si mtumba na yule anayedai hivyo aulizwe vyanzo vya taarifa hizo.

“Mabehewa yalianza kutengenezwa kwa miaka miwili, katika ununuzi kuna sheria tunaifuata ambayo lazima kabla ya kusema hii ndio tunaenda nayo kuna ulinganifu wa bei mbalimbali na kwa maana ya uhitaji wetu inaendana.


"Sasa mtu anavyoibuka na kuanza kulinganisha na kusema mabehewa yana kiasi fulani ni jambo la ajabu kidogo,” amesema.

Kadogosa amesema mabehewa hayo kwa awamu ya kwanza yameletwa 14 na mwakani mengine 45 yatawasili nchini na kufikia idadi ya mabehewa 59 yaliyoagizwa.

Ameeleza kuwa bei ya mabehewa hayo ni dola 59.6 milioni na taratibu zote za manunuzi zimefuatwa kuanzia uengenezaji mpaka mabehewa hayo kuwasili nchini.


Kupitia akaunti yake ya Twitter, Dk Kigwangalla pamoja namengine amedai kuwa bei ya kununua mabehewa hayo haina uhalisia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad