Boss wa SimbaTry Again Afunguka "Simba ipo katika mikono salama"




Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba SC Salim Abdallah ‘Try Again’ ametuliza hali ya hewa ndani ya Klabu hiyo, baada ya aliyekua Afisa Mtendaji Mkuu ‘CEO’ Barbara Gonzalez kutangaza kujiuzulu.

Barbara akithibitisha kujiuzulu juzi Jumamosi (Desemba 10), na kuzua taharuki kwa Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo ambao walihoji maswali mengi katika Mitandao ya Kijamii kuhusu kuondoka kwa kiongozi huyo.

Tyr Again amesema kuondoka kwa Barbara hakutaharibu lolote ndani ya Klabu hiyo na badala yake mazuri yoteyataendelezwa na kufikiwa kwa lengo linalokusudiwa msimu huu 2022/23.

“Simba ni Klabu kubwa haitabadilika eti kwa sababu CEO ameamua kujiuzulu nafasi yake, Simba itaendelea kuwepo na kufanikisha mipango yake kwa sababu ina uongozi unaofahamu dira yake,”

Simba SC ni Klabu kubwa Barani Afrika, hiki kilichotokea ni upepo mbaya ambao ni kawaida kupitia popote pale, lakini niwahakikishiea Wanachama Klabu yao ipo salama na itaendelea na mipango yake kama kawaida.” amesema Try Again

Amesema kwa sasa wapo katika mikakati ya kuiandaa timu yao kuelekea hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika lakini pia wanaendelea na mchakato wa kuimarisha kikosi kwenye Dirisha Dogo, ili kiweze kufanya vizuri katika Michuano wanayoshiriki msimu huu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad