Brazil Yatinga Robo Fainali Kombe La Dunia, Yashinda 4-1 Katika Uwanja Wa 974 Doha

 



Timu ya Brazil imeingia kwa kishindo katika robo fainali ya kombe la dunia baada ya kuifunga Korea Kusini mabao 4-1 katika uwanja wa 974 mjini Doha.


Alikuwa ni Venicius Jr aliyeandika bao la kwanza katika dakika ya 7 ya mchezo huo na Neymah Jr, aliyerudi baada ya kukosa mchezo uliopita akiwa majeruhi alipachika bao la pili katika dakika ya 13 naye Richarlison aliongeza bao la tatu katika dakika ya 29 na Lucas Paqueta alimalizia bao la 4 katika dakika ya 36.


Kwa upande wao Korea Kusini walipata bao la kufutia machozi katika dakika ya 76 Paik Seung-Ho.


Sasa Brazil inajiandaakukumbana na Croatia katika robo fainali siku ya ijumaa


Baada ya Japan kupoteza kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Croatia mapema, na Australia kupoteza mechi kwa Argentina, kushindwa kwa Korea Kusini kunamaanisha kwamba timu zote tatu za Shirikisho la Asia zimetolewa katika raundi ya kwanza ya mtoano.


“Wacha tuendelee na matumaini ya kushinda tutaendelea kucheza hadi fainali, “Vinicius Jr alisema. “Na pia tunamkumbatia Pele. Tutegemee atapona haraka.”


Croatia yatinga robo fainali baada ya kuitoa Japan kwa penati


Croatia ilikata tiketi yake ya kucheza tena robo fainali ya kombe la dunia baada ya kuitoa Japan kwa njia ya penati katika uwanja wa Al Janoub Doha Qatar.


Japan ilikuwa ya kwanza kupata bao lake kupitia kwa Daizen Maeda katika dakika ya 43.


Lakini bao hilo halikudumu kwa muda mrefu kwani Ivan Persic alisawizishia Croatia katika dakika ya 55.


Na hadi mwisho wa mchezo walibaki sare na hadi dakika za nyongeza hawakufungana na moja kwa moja kuelekea katika penati, ambapo walitolewa kwa jumla ya penati 3-1.


Japan waytaendelea kulumbukwa kwa usafi wao kwani kila baada ya mechi walibaki na washabiki wao kusafisha uwanja.


Hatukuweza kuvuka Raundi ya 16, na hatukuweza kuwa na mtazamo mpya au kuona mandhari mpya, lakini timu ya taifa ya Japan ilishinda dhidi ya Ujerumani na Uhispania, ambao wamekuwa mabingwa katika Kombe la Dunia Kocha wa Japan Hajime Moriyasu alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari.


Wawakilishi pekee wa Afrika waliobaki katika michuano hii Morocco wanapanda uwanjani Jumanne kupambana na Spain katika raundi ya pili huku wakiangaliwa kwa jicho la pekee na bara hilo.


Katka mchezo mwingine Ureno watapambana na Uswissi kuwania nafasi ya kuingia robo fainali ya mwaka huu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad