Cameroon Yavunja Mwiko, Yawa Timu ya Kwanza Kutoka Afrika Kuifunga Brazil




Timu ya taifa ya Cameroon imeipiga Brazil katika mechi yao ya mwisho ya kundi G kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar
Kocha wa Cameroon alikuwa ameapa kuipiga Brazil na kweli ametimiza ahadi yake kwa mashabiki wa Indomitable Lions
Cameroon imekuwa timu ya kwanza ya Bara Afrika kuicharaza Brazil katika mashindano ya Kombe la Dunia

Timu ya taifa ya Cameroon imeicharaza Brazil katika mechi yao ya mwisho ya kundi H kwenye mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini Qatar.


The Indomitable Lions chini ya ukufunzi wa mchezaji wao wa zamani lejendari Rigobert Song imeitandika Brazil 1-0; timu inayoorodheshwa nambari moja duniani na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Vincent Aboubakar afunga na kupata kadi nyekundu
Nahodha wa Cameroon Vincent Aboubakar alifunga bao hilo kwa kichwa katika muda wa zaida wa kipindi cha pili lakini akapata kadi ya pili ya njano kwa kuvua shati lake.



Aboubakar ameandikisha historia kama mchezaji wa tatu wa taifa la Afrika kufunga Brazil katika Kombe la Dunia baada ya Didier Drogba (Ivory Coast 2010) na Joel Matip (Cameroon 2014).


Rigobert Song aahidi kuipiga Brazil
Brazil iliingia katika mechi hiyo ikijivunia rekodi nzuri zaidi katika safu ya ulinzi kwani ilikuwa bado haijaruhusu kufungwa hata golo moja.

Kocha Song hata hivyo alikuwa ameapa kuipiga Brazil na kweli ametimiza ahadi yake kwa mashabiki wa Indomitable Lions.

"Tunaamini tunaweza kulifanya dhidi ya Brazil. Hatukuja kwenye Kombe la Dunia kuongeza idadi ya timu tu, hapana," Song alisema.
Cameroon imekuwa timu ya kwanza ya Bara Afrika kuicharaza Brazil katika mashindano ya Kombe la Dunia.

Ushindi huu hata hivyo haujatosha kuwapeleka katika raundi ya 16 kwani wamemaliza katika nafasi ya tatu kundi H nyuma ya Brazil na Uswizi huku Serbia ikiwa ya nne.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad