Staa wa Muziki wa RnB, aliyetamba na Ngoma ya 'My Heart Will Go On' , Celine Dion (54) amefunguka kuwa kwa sasa hali yake sio nzuri baada ya kugundulika kuwa na hali inayoitwa 'Stiff Person' Syndrome (SPS), yenye sifa za ugonjwa wa autoimmune ambapo misuli inakuwa inakaza.
Mwimbaji huyo wa Kifaransa wa Canada aliwaambia wafuasi wake milioni 5.2 kwenye mtandao wa Instagram hali hiyo inamfanya misuli yake ikaze bila kudhibitiwa. Pia imemfanya kuwa na ugumu wa kutembea na kuimba, alisema, akimaanisha kuwa hataweza kushiriki maonesho yaliyopangwa nchini Uingereza na Ulaya mwaka ujao.
"Nimekuwa nikikabiliana na matatizo ya afya yangu kwa muda mrefu," Dion alisema. "Na imekuwa vigumu kwangu kukabiliana na changamoto hizi na kuzungumza kuhusu kila kitu ambacho nimekuwa nikipitia," Alieleza katika video iliyojaa hisia.
"Wakati bado tunajifunza kuhusu hali hii adimu, sasa tunajua hii ndiyo imekuwa ikisababisha mifadhaiko yote ambayo nimekuwa nayo." Aliongeza: "Kwa bahati mbaya, kukaza huku kunaathiri kila nyanja ya maisha yangu ya kila siku, wakati mwingine husababisha ugumu ninapotembea na kutoniruhusu kutumia sauti zangu kuimba jinsi nilivyozoea.
"Inaniuma kukwambia leo kwamba hii inamaanisha kuwa sitakuwa tayari kuanza tena ziara yangu huko Ulaya mwezi Februari."
"Timu kubwa ya madaktari wanaofanya kazi pamoja nami ili kunisaidia kupata nafuu" huku "watoto "wakiniunga mkono na kunipa msaada".