Uamuzi wa Fernando Santos kumtupa mkekani nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia, ulizaa matunda kwani mshambuliaji Goncalo Ramos aliyerithi nafasi hiyo alifunga bao la kifundi dhidi ya Uswizi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, alifunga bao la kustaajabisha katika dakika ya 17 na kuiweka timu yake kifua mbele na 1-0 kwenye Uwanja wa Lusail mnamo Jumanne, Novemba 11 usiku.
Bao hilo lilikuwa la kwanza la Ramos kwa Ureno katika Kombe la Dunia na bao lake la pili la kimataifa kwa jumla.
Ramos alifunga bao lake la kwanza kwa nchi yake katika mechi ya kirafiki dhidi ya Nigeria mnamo Novemba 17, 2022, ambapo Ureno ilishinda 4-0.
Ramos aliendeleza kiwango chake bora kwenye pambano hilo kwa akimalizia vyema krosi ya Diogo Dalot dakika sita baada ya kipindi cha mapumziko, akimbwaga Raphael Guerriero kuongeza bao lake la pili.
Beki wa Manchester City, Manuel Akanji aliifungia Uswisi bao moja lakini Ramos akapata la tatu kwa haraka kwa kutumia ujanja ambao ulikuwa ishara kwa umati kumtambulisha Ronaldo.
Ronaldo alipachika mpira wavuni lakini ilikataliwa kwa msingi wa kuotea huku mwenzake Rafael Leao mwenye umri wa miaka 23, akifunga bao la sita huku Ureno ikitwaa ushindi wa 6-1.
Cristiano Ronaldo aliachwa akisugua benchi wakati wa mechi muhimu ya Ureno ya raundi ya 16 dhidi ya Uswizi.
Hatua hiyo mpya ilitokana na ripoti kwamba meneja wa Ureno, Fernando Santos hakufurahishwa na Ronaldo kwa ishara yake wakati wa kushindwa na Korea Kusini.
Siku ya Ijumaa, Ronaldo alitolewa katikati ya kipindi cha pili na alipokuwa akiondoka, aliweka kidole chake cha shahada mdomoni kana kwamba anamwambia mtu "nyamaza".