Cristiano Ronaldo Kujiunga na Klabu ya Saudia ya Al Nassr Mwishoni mwa Mwaka




Klabu ya Saudi Arabia ya Al Nassr inatarajia kupata saini ya mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo mwishoni mwa mwaka huu.


Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United atasaini mkataba wa miaka miwili na nusu wenye thamani ya £174m (KSh26.1 bilioni).

Kwa mujibu wa gazeti la Marca, kwa sasa mshambuliaji huyo hodari mwenye umri wa miaka 37, yuko nchini Dubai akitazamiwa kusafiri kuelekea Saudia.


Ronaldo pia ameweka nyuma masaibu ya Kombe la Dunia na amemaliza mazoezi yake mjini Valdebebas nchini Uhispania.


Mazungumzo ya kujiunga na klabu hiyo ya Saudia yalianza punde baada ya kuondoka kwake Manchester United.

Kutua kwa Ronaldo nchini Saudia kunachukuliwa kupiga jeki serikali ya taifa hilo kuonekana kwenye ramani ya soka ya kimataifa kwani nchi hiyo inaazimia kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la 2030.

Mradi huo unalenga kuwapa umaarufu mkubwa zaidi katika ulimwengu wa michezo, kama tayari wanavyojivunia katika soka wakiwa na Spanish Super Cup, Formula 1, gofu, na mbio za farasi kwa kiwango cha juu zaidi.

Cristiano anachukua fursa ya likizo ya Krismasi kupiga unyunyu siku chache nchini Dubai.


Hii ni baada ya michuano ya Kombe la Dunia kuwa pigo kubwa kwa Mreno huyo hususana kutokana na ushindi wa Argentina na mpinzani wake mkubwa Lionel Messi.

Hata hivyo, anaonekana bado hajakata tamaa kwani hajatangaza kustaafu soka la kimataifa na kuagana na timu ya taifa ya Ureno.

Kinachoonekana wazi ni kwamba vilabu ya soka laUlaya vimemkataka kutokana na uzoefu wake akiwa Juventus na Manchester United.


Lakini sasa ana kibarua kigumu kinachomsubiri cha kupiga jeki Saudi Arabia kuonekana katika ramani soka la dunia.

Ronaldo anatarajiwa kutia saini mkataba na Al Nassr hadi Juni 2025.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad