Eric Omondi Awachana Wasanii wa Kenya "Harmonize Amekuja Tamasha la Sauti Sol Lakini Kila Mtu Anajua Yeye Ndio Kaandaa Hiyo Show"


Mchekeshaji Maarufu Nchini Kenya @ericomondi Azidi kulia na Uwekezaji unaofanywa na Wasanii wa Nchini Kenya na Wasanii wa Tanzania huku akitolea Mfano Wasanii wawili waliotoa Burudani kwenye Tamasha la #SolFest ambao ni @harmonize_tz na @nadia_mukami Huko Nchini Kenya.

#Omondi Amesema kuwa Msanii @harmonize_tz ametumia muda wake kuandaa timu ambayo ameibeba kutoka Tanzania mpaka Nairobi, Kenya akiwemo Mpiga picha ambapo ameweka video Tatu zikionesha matukio yote ya utumbuizaji wake kwenye Tamasha hilo ambapo Mashabiki zake baadhi wanadhani Show hiyo iliandaliwa na #Harmonize pekee na kuudhuriwa na watu 15,000
Mbali na hilo #EricOmondi ametolea Mfano Msanii kutoka Nchini Kenya #Nadia ambae anadai ni Miongoni mwa wasanii waliotumbuiza Vizuri zaidi kwenye Tamasha la #SolFest lakini kwenye Mitandao yake ya Kijamii ameweka Picha akiwa kwenye Ukuta usio eleweka kitu ambacho kimefanya Mashabiki zake kushindwa kuelewa kama alitumbiza katika Show hiyo. Na kusema kuwa hiyo inaweza msababishia kukosa madili.
.
.
Una Maoni gani kwenye hili?

SWIPE LEFT...
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad