Fei Toto Afunguka "Umekuwa wakati mzuri sana kuichezea klabu ya Young Africans"




Umekuwa wakati mzuri sana kuichezea klabu ya Young Africans SC

(Yanga) klabu yenye historia kubwa na ya kuvutia nchini na Afrika yote. Tumekuwa na nyakati nyingi mchanganyiko, tulifurahi pamoja pale furaha ilipokuja uelekeo wetu na tulihuzunika pamoja nyakati mbaya zilipotutokea.

Nitakumbuka mengi mazuri yaliyotokea pamoja na nitasahau yote mabaya kwa haraka sana.

Kila nikiwakumbuka mashabiki wa WANANCHI moyo unakua mzito kuwaaga, hivyo hivyo kwa wachezaji wenzangu na viongozi pia kwa upendo mlionionyesha tukiwa pamoja kwenye shida na raha. Lakini lisilo budi hutendwa au hunenwa kwahiyo leo nasema KWAHERINI WANANCHI.

Ila maisha ndivyo yalivyo mambo huja na kupita na kuna wakati yanajirudia, mpaka wakati mwingine tena, Kwaheri ya kuonana.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad