Imeripotiwa kuwa Fifa inachunguza jinsi mpishi maarufu Salt Bae na watu wengine kadhaa walipata nafasi isiyofaa kufika ndani ya uwanja mwishoni mwa fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar na kulishika kombe.
Salt Bae ambaye jina lake halisi ni Nusret Gokce ni mpishi wa Uturuki, alionekana katika picha akiwa ameshika na kubusu kombe la Dunia akisherehekea na wachezaji wa Argentina baada ya ushindi wao dhidi ya Ufaransa.
Sheria za Fifa zinasema kombe hilo linaweza tu kushikiliwa na kundi la watu walioidhinishwa pekee, wakiwemo washindi wa mashindano, maafisa wa Fifa na wakuu wa nchi.