Watu Watano wamefariki dunia papo papo eneo la Mikumi Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro katika ajali iliyohusisha gari ndogo IT yenye namba za usajili IT 6954 DNN iliyokuwa ikitokea Jijini Dar-es-salaam kuelekea mpakani Tunduma baada ya kugongana uso kwa uso na gari kubwa la mafuta aina ya Benzi lenye namba za usajili RL 2686 iliyokuwa ikitokea Mkoani Iringa kuelekea Mkoani Morogoro.
Kwa mujibu wa kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Morogoro, Fortunatus Musilim amesema ajali hiyo iliyotokea majira ya usiku wa kuamkia leo eneo la Iyovu wilayani Kilosa Mkoani Morogoro barabara kuu ya Morogoro-Iringa huku sababu ikitajwa kuwa ni uzembe wa dereva wa gari ndogo.