Gharama zilizo tumika kufikia kwenye pambano hili ni kubwa sana..maumivu waliyopitia mabondia kwenye maandalizi ya pambano hili ni makubwa sana, hamu ya mashabiki kuelekea pambano hili ilikua kubwa sana pia.
Kwa pambano ambalo limesubiriwa kwa miaka mingi ni fedheha kubwa kuisha kwa namna hii, ni kama kuunajisi mchezo wa ngumi.
Mpasuko aliopata Piallali sio wa kumaliza mchezo hata kidogo, ila kutokana na maandalizi duni kwenye kitengo cha utabibu kimepelekea mchezo kuvunjika. Kuna mipasuko mikubwa zaidi ya hii hutokea kwenye boxing na mchezo huendelea baada ya matibabu sahihi kupatikana.
Sio mara ya kwanza linatokea..fight ya Kidunda vs Katompa yalitokea haya haya na leo tena yana tokea.
Ukienda picha ya inayofuata ni Tuson Fury alipata huo mpasuko kwenye mechi dhid ya Otto Wallin lakini fight haikuishia hapo.
Leo hii huku Pialali anapata cut doctor na kona ya bondia wanaulizana mafuta yako wapi na hakuna mwenye majibu, unategemea utaweza kuzuia hiyo damu kutoka?
Watu wanalipa viingilio, ving'amuzi, wanasafiri kwaajili ya hizi fight kwanini hatujali kwa kuweka mazingira bora ya kuthamini pesa zao? NI FEDHEHA.