Mwanamitindo na mwanamuziki mashuhuri wa Bongo Hamisa Mobetto amekiri upendo wake mkubwa kwa mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe.
Mobetto alidokeza kuwa anavutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kwenye Instagram na kudai kwamba anajifunza Kifansa kwaajili yake.
"À se damner🥰 (Nakukufia)," aliandika kwenye ukurasa wake.
"Najifunza kifaransa kwaajili ya #mbappe," alieleza.
Mama huyo wa watoto wawili aliambatanisha ujumbe huo na picha yake nzuri inayoonyesha akiwa ameshika tumbo lake huku akiwa anawaza.
Mobetto ni miongoni tu mwa wanadada wengi ambao wametekwa moyo na mshambuliaji huyo wa PSG hasa baada ya mchezo wake mzuri katika fainali ya Kombe la Dunia ambayo ilifanyika siku ya Jumapili ugani Lusail, nchini Qatar.
Licha ya Ufaransa kupoteza, Mbappe alikonga nyoyo za wengi kutokana na uchezaji wake mzuri kwenye mechi dhidi ya Argentina ambapo alifunga mabao manne. Pia alipewa tuzo la mfungaji bora baada ya kumaliza mashindano hayo na mabao nane.
Kufuatia ubabe alioonyesha, mamilioni ya wanadada wamekuwa wakimmiminia sifa kemkem mwanasoka huyo huku wengine wakikiri hisia zao kwake.
Mwezi uliopita, mpenzi huyo wa zamani wa staa wa Bongo Diamond Platnumz pia alikiri upendo wake kwa muigizaji wa Marekani Michael B. Jordan.
Kwenye akaunti yake ya tiktok, mama huyo wa watoto wawili alichapisha video ya mkusanyiko wa picha kadhaa za Jordan na kumtambulisha kama mwanamume ambaye angetaka kuolewa naye.
"Ona mvulana ninayetaka kuolewa naye 😩❤️💍👉🏼" aliandika chini ya video hiyo iliyoanza na picha yake.
Hapo awali, Hamisa Mobetto alitangaza wazi kuwa amezama kabisa kwenye dimbwi la mahaba.
Katika video aliyochapisha mitandaoni, mzazi mwenza huyo wa staa wa Bongo Diamond Platnumz alikiri mapenzi yake mazito kwa mpenzi wake mpya na kufichua kuwa yuko tayari kufunga ndoa naye.
"Hatimaye nimepata mtu. Nimepata mwanaume ambaye nahisi ni yeye nataka. Nahisi kama kwamba huyu ndiye mtu ningependa kushiriki maisha yangu yote naye," alisema kwa kujivunia na msisimko mkubwa.
Mobetto aligamba kwamba hatimaye amefanikiwa kupata mwanamume anayezungumza lugha ya mapenzi sawa na yeye.
"Kila kitu ni rahisi sana, kila kitu ni sawa" alisema.
Aidha alisema kuwa anatamani sana kuvishwa pete na mpenzi wake mpya na kuchukua majukumu ya mke.
"Nataka kuolewa naye. Nataka kuolewa na mtu wangu. Nataka kumpikia, nimuandalie nguo ili aende kazini. Je, hii ni ndoto? niamke? Ikiwa ni ndoto mtu tafadhali anichune niamke," alisema Mobetto.
Ingawa hakumtambulisha mpenziwe, Mobetto alimsifia sana na kusema kuwa yeye ndiye mume kamili kwake.
Kuwa wa kwanza kutoa maoni
Hamisa Mobetto akiri mahaba kwa Mbappe, asema anajifunza Kifaransa kwa ajili yake
radiojambo.co.ke
1h
"Najifunza kifaransa kwaajili ya #mbappe," Mobetto alieleza.
Muhtasari
•Mobetto alidokeza kuwa anavutiwa na Mbappe kwenye Instagram na kudai kwamba anajifunza Kifansa kwaajili yake.
•Aliambatanisha ujumbe huo na picha yake nzuri inayoonyesha akiwa ameshika tumbo lake huku akiwa anawaza.