MSANII Rajabu Kahala ‘Harmonize au Harmo’ baada ya kuachana na Kajala Masanja, wiki iliyopita alionyesha jinsi anavyompenda Christina Shusho ambaye ni msanii wa nyimbo za injili.
Harmo amemtaja Shusho kuwa ni msanii bora, mwenye heshima zaidi nchini, alisema hayo baada ya kukutana ana kwa ana na msanii huyowa injili.
Ili kuonyesha kwamba Harmo anamzima Shusho, aliibusu miguu ya msanii huyo mwenye sauti nyororo, kisha akamkumbatia kumpongeza.
Harmo amesema: “Navutiwa na sauti yake, mpangilio wa nyimbo zake na jinsi anavyofanya kazi zangu kwa kuzingatia maadili yanyimbo anazoimba.” Shusho ambaye amejaliwa na Mungu uwezo wa kutungana kuimba nyimbo za injili na amefanikiwa kuwa na mashabiki wengi mitaani na hata kwenye mitandao ya kijamii.
Msanii Rajabu Kahala ‘Harmonize au Harmo.
Baadhi ya ngoma ambazo zimemletea sifa katika muziki wake ni ‘Teta Nao’, ‘Shusha Nyavu’, ‘Relax’, ‘Ushirika na Wewe, ‘Mwanga’, ‘Litapita’.
‘Muujiza’ na kadhalika. Hata hivyo, upendo wa Harmo kwa Shusho umetajwa kwamba unahusu muziki tu na si vinginevyo kwani mwanamama huyo yupo kwenye ndoa. Wachambuzi wengine wa mambo ya wasanii wanasema jambo linalotia shaka ni tabia ya Harmo ambayo haiaminiki hasa anapokuwa na urafiki wa kirafiki na mwana dada.
Harmo aliwahi kutoa kolabo na mwanamama Jane Misso katika wimbo wa Yomoyo Remix ambapo ngoma hiyo ilikoga nyoyo za watu akiwemo Nabii Mkuu Geordevie wa Arusha ambaye alitaka kumzawadia Harmo gari baada yakufurahishwa na ngoma hiyo. Geordavie alisema alisikia ngoma hiyo ghafla na kushituka baada ya kufurahishwa nao na akawauliza mtu ambaye alitengeneza ngoma hiyo.
Alipoambiwa ni Harmo alishangaa kuona mtu wa Bongo Fleva kuweza kuandika na kuimba wimbo huo ambao ulikuwa unamsifu Mungu na kupangiliwa vizuri. Licha ya mtumishi huyo wa Mungu; mjadala mzito pia uliibuka baada ya Harmo na mwanamama huyo kutoa wimbo huo huku wengine wakidai kwamba kutokana na tabia yake Harmo hakupaswa kuimba ngoma hiyo yakumsifu Mungu.
Hata hivyo; kuna viongozi wengine wa dini wanasema tabia ya mtu haimzuii kumsifu na kumtangaza Mungu kwani wapo viongozi wa dini wanaoaminika na wanaojulikana, wana tabia mbaya lakini wanahubiri maneno ya Mungu.
Harmonize amekuwa anatajwa kutoaminika kwa wanawake huku wakitoa mfano jinsi walivyokosana na Kajala mara ya kwanza baada ya kugundulika kuwa alikuwa ‘akimzengea’ mwanaye, Paula.
Kitendo hicho kilizua gumzo na kusababisha makubwa kwa wawili hao kwani walitengana huku Paula akimwaga mboga kwa kuonyesha meseji zote ambazo Harmo alikuwa akimtumia kumtongoza. Harmo pia alikosana na mchumba wake Sarah kutokana na kudaiwa kuwa hakuwa mwaminifu katika uchumba wao. Kwa upande wa mwingine; haijajulikana nini kitafuata baada ya hili lililotokea kwa Shusho; kwamba ama kuna muziki utatengenezwa kati ya wawili hao au vipi. Tusubiri tuone.
MAKALA; ELVAN STAMBULI, DAR