Mwaka 2022 umekuwa mwaka mzuri kwa tasnia ya muziki wa Tanzania, tukishuhudia kuibuka kwa wasanii mbalimbali wanaochipukia, wasanii wakijituma zaidi ya kawaida kwenda kwenye viwango vya juu na kutambulika kimataifa. Mwaka umeshuhudia wasanii takriban sita wa Tanzania wakijiunga na ‘Boomplay Golden club’.
Hii ni klabu mahususi kwa wasanii waliopata wasikilizaji zaidi ya milioni mia moja Boomplay huku Tanzania ikiwa nchi ya pili kwa kuwa na wasanii wengi baada ya Nigeria.
Katika kufunga mwaka huu mzuri katika tasnia ya muziki, App namba moja kwenye utoaji wa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki barani Afrika, Boomplay, imetoa takwimu zake za kila mwaka ambazo zimekuwa zikisubiriwa kwa hamu yaani #BoomplayRecap2022
@boomplaymusic_tz imewataja wanamuziki watatu wa kiume toka hapa nchini walioongoza kusikilizwa mwaka huu (2022) kwenye App hiyo. Kwa mujibu wa Boomplay wanamuziki hao ni @diamondplatnumz @harmonize_tz na @marioo_tz kwa kuzingatia idadi zao za streams kuanzia tarehe 1/11/2021 hadi 30/10/2022