Kupitia ukurasa wake wa #twitter mchekeshaji @idrissultan ameshare mkasa uliompata siku mbili zilizo pita wa kuvamiwa nyumbani kwake na mwanamke anayedhaniwa kuwa na matatizo ya akili huku mwanamke huyo akidai Idriss ndiye sababu ya yeye kuwa kichaa, lakini pia anamdai shilingi elfu 50, ila haitaki hiyo pesa, alichofuata kwake ni tendo la ndoa.
“Nipo ndani ya nyumba yangu siwezi kutoka sababu kuna mwanamke amevamia kwangu amesema nimesababisha amekuwa kichaa. Kasema ananidai elf 50 ila kabadili mawazo haitaki tena, anataka tucheze mchezo(akaashiria ngono). Nimepiga simu polisi ndo nasubiri wafike 😰 #SioMasihara” Tweet 1
“Mapolisi wapo njiani, for some reason amekaa kwenye compound yangu anasikiliza nyimbo za Joel Lwoga” tweet 2
“Alhamdulillah, ameshaondoshwa. Shukran sana Polisi kwa msaada wenu mkubwa. I hope atapata msaada anaohitaji kiakili.”
“Update: Polisi station alikuwa mtulivu hakuna njia ya ku-prove kama hayupo sawa kwa muda huo ma mimi nikaona sio sawa kufungua mashtaka kwa mtu ambaye ni wazi kuna tatizo kwenye mental health. Akaachiwa. Saa kumi na moja asubuhi karudi kwangu kagonga mageti yote akaondoka 6am😰”
“Update 2: Kesi ipo polisi tutatafuta jinsi ya kumsaidia. Alifika tena nyumbani kwangu mara ya tatu akazuiwa. Akatupa chupa juu ya geti na madawa kama unavyoona kwenye picha kisha akaondoka. Jamii yetu imezoea kuwa mwenye matatizo ya afya ya akili ni mchafu na anakesha jalalani.”
“Update 3: Currently sijui kaingia vipi kwenye geti, katupa simu ndani kwangu tukawahi kufunga vioo ndo hiyo lolipop imeishia kwenye dirisha. Nimekaa tena nasubiri polisi wafike hoping yupo huko nje apelekwe hata hospitali. This doesn’t even sound real nikitafakari🤦🏽♂️”
“Usiku kama saa nane tumefanikiwa kumfikisha Muhimbili kwa msaada wa dada yake na watu mtaani kwetu. Polisi wamesema ameshawahi kuwakung’uta wafungwa wenzie haitakuwa salama kumshikilia mahabusu kusubiri hospitali. Asanteni sana kwa pole zenu na poleni kwa kuwafelisha wahuni 🙄”
#sajomedia #entertainment #idrissultan
23 MINUTES AGO
Post