Kajala Masanja amekuwa gumzo katika vyombo mbalimbali vya habari baada ya kutengana na msanii maarufu wa bongo fleva Harmonize.
Wawili hawa mwezi Juni mwaka huu waliweza kuvishana pete ya uchumba na kuahidi ndoa kubwa kuja baada ya tukio hilo kumalizika.
Kajala ni mpambanaji sana katika kuyatafuta mafanikio nje ya maisha ya Sanaa yake. Machi 25, 2013, aliachiwa huru baada ya kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kutakiwa kulipa faini ya Tsh 13,000,000.
Hukumu hiyo ni kutokana na kesi iliyokuwa inamkabili ya utakatishaji wa fedha, lakini msanii nguli Wema Sepetu alimlipia faini hiyo na kuwa huru.
Mbali na Sanaa yake ya uigizaji na iliyomfanya atambulike vyema kwa mashabiki, kwa sasa haonekani sana huku ila amewekeza nguvu zake kwenye biashara mbalimbali zinazomfanya aishi mjini kwa furaha na amani.
Licha ya mafanikio aliyokuwa nayo ila ni mwanamke mvumilivu na anayejua kupenda na kuonesha mapenzi ya kweli.
Uhusiano wake wa kwanza aliouweka wazi ni wa Pfank Majani ambapo waliweza kupata mtoto mmoja wa kike ambaye ni Paula Kajala, naye kwa sasa amekuwa maarufu kutokana na skendo nyingi katika mitandao ya kijamii za uhusiano kati ya yeye na msanii maarufu Rayvan aliyekuwa chini ya lebo ya muziki WCB.
Nimekugusia tu kidogo kuhusu Paula, twenzetu tumjue zaidi mwanadada Kajala Masanja.
Baada ya hapo tukaona ameweka wazi uhusiano wake wakutoka na staa wa muziki Harmonize, kwa muda mfupi waliweza kuwa pamoja na wakaja kutofautiana, sababu zilizosemekana kuwa Harmonize alikuwa anajihusisha na uhusiano wa kimapenzi na binti wa Kajala (Paula) na kupelekea wawili hao kutofautiana kutokana na skendo hiyo.
Harmonize baada ya upepo huo kuvuma vibaya aliweka wazi katika mitandao yake ya kijamii na vyombo vya habari mbalimbali, kuomuomba msamaha mrembo Kajala na iwapo mwanadada Kajala atakubali kumsamehe atafunga naye pingu za maisha na kumfanya mkewe.
Lakini mambo kwa sasa yamegeuka tena wametofautiana na kila mtu kuchukua kilichokuwa chake na kusepa.
Hapa inaonesha ni mtu anayependa lakini pia anateswa na mapenzi kwa kuwa katika hali ya kawaida mapenzi mazuri ni yale ya kuwa na mmoja kwa muda mrefu.