Waandishi mbalimbali nchini Ufaransa wanadai kwamba wachezaji wengi kasoro Griezman na Lloris walikuwa upande wa Karim Benzema huku wakihitaji arejee ila Kocha Deschamps na shirikisho la soka wakiongozwa na Rais Le Graet walikuwa wanapinga ikiambatana na kuwaonya Wachezaji juu ya kusimama upande wa Benzema.
Karim kususia mwaliko wa Rais haikuwa bahati mbaya hata Zidane kususia haikuwa bahati mbaya, mengi ya chini kwa chini yanaendelea kwenye kikosi hicho kwa mujibu wa Waandishi.