Kigwangalla "Nipo Tayari Kuwekeza Simba Nitatafuta Namna"


Mbunge wa Nzega Vijijini na mwanachama wa Klabu ya Simba SC na Dk Hamisi Kigwangalla kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram ameandika

”Sijui kuna kitu gani kinaendelea ndani ya klabu yetu ya Simba. Sijui kwa uhakika, lakini nasoma comments za wadau/washabiki wa Simba kwenye kurasa zangu za mitandao ya kijamii na wengine wakichukua muda wao kuniandikia meseji kabisa.”

”Baadhi wakitaka nigombee uongozi ndani ya Simba, na wengine wakinisimanga kuwa ninunue hisa za Simba sasa kwa kuwa tajiri anauza hisa zake!”

”Kuhusu kugombea nafasi yoyote ile ya uongozi ndani ya Simba, jibu langu mara zote limekuwa HAPANA! Kiukweli, sijawahi kutamani kuwa kiongozi wa Simba hata mara moja. Mimi ni mshabiki na mwanachama tu. Itabaki kuwa hivyo.”

”Kitu cha wengi lazima kiwe na maneno tu, sababu ni cha wengi. Usitegemee watu watanyamaza. Wabunge tunasemwa kila siku, why? Sababu ni mali ya umma, tumetaka wenyewe. Hata muwekezaji wetu angetaka asisemwe angeanzisha klabu yake kama Mzee Bakhresa tu, wala asingetusikia kumsema.”

”Ukitaka kuchukua hisa za klabu kama Simba ni lazima uwe mkweli, muwazi na serious kidogo. Ukileta janja janja tutakuvumilia kidogo mwisho tutasema. Klabu yetu ina maslahi ya umma na ni lazima tutayalinda siku zote. Kama siyo Kilomoni, basi ni Kigwangalla, ama Kingwendu.”

”Kama kweli muwekezaji ameshindwa kuwekeza, na anataka kuondoka, menejimenti ya Simba waweke wazi, wanasimba tutaamua. Siyo kuleta vijembe.”

”Mimi sijawahi kufikiria kuwekeza kwenye mpira lakini nikilazimika kufanya hivyo, niko tayari kufikiria na kutafuta namna.”


”Aidha, ninajitolea bure kuwa Consultant wa Simba kwenye eneo la uwekezaji, mikakati na masoko, menejimenti, uongozi na usimamizi katika kipindi cha mpito, kama kweli muwekezaji anaondoka.”

”Simba haipaswi kutetereka mpaka kiasi cha kuzua taharuki juu ya bus tu, kama kweli tumenyang’anywa; haswa ikizingatiwa mikataba ya matangazo na wadau tuliyonayo, achilia mbali mauzo ya jezi, viingilio na wafadhili wengine.”

”NB: Muwekezaji hakuwahi kulipia hisa zake, hivyo hana haki ya kusema ‘anauza’ hisa. Kuhusu ufadhili aliotoa, binafsi kama mwanasimba, namshukuru na kumpongeza kwa juhudi hizo, hata hivyo haikuwa bure sababu hatujui alikuwa akifaidika vipi kwenye matangazo ya bidhaa zake. ”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad