Waziri wa Zamani na Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla, kupitia Mtandao wa #Twitter amehoji sababu za Shirika la Reli Nchini (TRC) kununua Mabehewa ya Mradi wa Treni ya Umeme (SGR) ambayo yamekwishatumika
Amesema “Hili Behewa moja (tena used) limenunuliwa kwa Tsh. ngapi? Tumeambiwa yapo Mabehewa 54, yamenunuliwa kwa Dola za Marekani Mil. 59. Kwahiyo behewa moja ni Dola 1,092,592 ambayo ni sawa na Tsh. 2.57 Bil. Hivi hizi ni taarifa za kweli ama? Yamekuja 14 ya awali, bado 45. Kwanini wametununulia used?”
Ameongeza, "Mama (Rais Samia) hahusiki kwenye ununuzi wa Mabehewa, hao ni Watu wetu wa TRC tu. Na Ndiyo maana tunahoji kwa Uhuru kabisa! Watoe majibu. Najua Mama yuko na sisi, tunachofanya ni kumsaidia kazi ya kuwawajibisha Watu wajanja wajanja! Peke yake hawezi kufanya yote haya!"