Kilogramu 46 za bangi zakamatwa



Jeshi la Polisi mkoa wa Ruvuma limekamata bangi magunia matatu yenye uzito wa kilogramu 46 na miche ya bangi iliyolimwa kwa kuchanganywa kwenye bustani ya mbogamboga pamoja na na nyara za serikali yakiwemo meno ya Tembo saba sawa na Tembo wanne.

Akielezea matukio hayo Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma  ACP Marco Chillya, amesema jeshi la polisi lilifanya misako mikali katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Ruvuma na kufanikiwa kukuta bangi magunia matatu yenye uzito wa kilogramu 46 pamoja na miche ya bangi ambayo ililimwa kwa kuchanganywa kwenye bustani ya mbogamboga.

Katika misako hiyo kamanda Chillya amesema jeshi la polisi lilifanikiwa pia kukamata nyara za serikali yakiwemo meno ya Tembo saba sawa na Tembo wanne ambao wameuawa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad