Licha ya ubora wake katika kipindi chote cha pambano, Mbappe alishindwa kuzuia hisia zake akishuhudia Argentina wakisherehekea ushindi wao wa Kombe la Dunia.
Kylian Mbappe alithibitisha ni kwa nini jina lake linapaswa kutajwa katika kiwango sawa na Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kufuatia mafanikio yake ya ajabu katika fainali ya Kombe la Dunia.
Fowadi huyo wa Paris Saint-Germain alifunga mabao manane katika michuano hiyo ya dunia iliyokamilika Jumapili, Disemba 18, ikiwa ni pamoja na kufunga hatrick katika fainali dhidi ya Argentina.
Licha ya umahiri wake wa kufunga mabao, juhudi zake ziliambulia patupu huku Argentina ikitwaa taji lao la tatu la Kombe la Dunia kupitia mikwaju ya penalti.
Mbappe alifunga bao la kifundi katika dimba hilo na pia mkwaju wa penalti mbil katika dakika 90 na dakika 30 za muda wa nyongeza.
Aliboresha zaidi hadhi yake ya mchezaji bora kwa kufunga penalti ya kwanza kati ya miwili ya Ufaransa iliyopigwa kwa mafanikio huku Argentina ikiilaza Les Bleus 4-2 katika mikwaju ya penalti.
Baada ya Kombe la Dunia kukunja jamvi katika njia yenye mvuto, fowadi huyo mwenye umri wa miaka 23, aliachwa akiwa na huzuni, akimtazama mchezaji mwenzake wa PSG, Leo Messi na wenzake wa Argentina wakisherehekea ushindi wao mnono.
Katika picha iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii, Mbappe aliyekuwa mwingi wa majonzi alifarijiwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye alimkumbatia mikononi mwake.
Mbappe na Rais Macron wana uhusiano wa karibu huku akiwajibikia kurefusha mkataba wake wa PSG, Daily Mail inaripoti.
Japo alipoteza Kombe la Dunia,Mbappe alishinda tuzo ya kiatu cha dhahabu kama zawadi ya kufuta machozi kwa umahiri wake wa kufunga mabao.
Mbappe alitwaa tuzo hiyo ya kifahari baada ya kuibuka mfungaji bora wa mbao katika Kombe la Dunia 2022 lililosaktwa nchini Qatar.
Staa huyo wa Paris Saint-Germain alifunga mabao manane ya ajabu wakati wa michuano hiyo, ikiwa ni pamoja na hat trick kwenye fainali dhidi ya Argentina Jumapili.