Kombe la Dunia Halina Mwenyewe Mwaka Huu, Afrika Yaingiza Timu Mbili 16 Bora


WORLD Cup 2022, mpaka hatua ya makundi imemalizika, hakuna timu iliyoshinda mechi zote.

Timu tatu tu hazijafungwa; Morocco, Holland na England.

Timu hizo zimeshinda mbili na sare moja; pointi 7@.

Leo tunaanza Knockout stage. Timu 13 zilizofuzu 16th round, zimeshafungwa angalau mchezo mmoja.

Tathmini; Kombe halina mwenyewe hili. Yeyote anaweza kubeba. Itategemea na jinsi timu itachanga karata zake.

Afrika; Matumaini kwa Senegal wanaoimarika au Morocco ambao hawajapoteza mchezo.

Morocco wameongoza Group F. Ni mara ya kwanza kwa Africa tangu Nigeria walipoongoza Group D mwaka 1998.

Nigeria walishaongoza Group Stages mara mbili; 1994 na 1998.

Ni mara ya pili Morocco kuongoza kundi. Mara ya kwanza ni mwaka 1986, walipoongoza Group F, lakini walitolewa 16th round na Ujerumani Magharibi.

Cameroon wamepata kuongoza kundi mara moja. Ni mwaka 1990, Group B. Walifika mpaka Robo Fainali na kutolewa na England.

Hii ni mara ya pili kwa Afrika kuingiza timu mbili 16th round. Mwaka 2014, Nigeria na Algeria zilifuzu, ingawa hakuna iliyofika robo.

Timu za Afrika ambazo zimewahi kufika angalau Robo fainali ni 3; Cameroon 1990, Senegal 2002 na Ghana 2010.

Afrika itajitafuta kesho kwenda Robo kwa England vs Senegal na Jumanne Morocco vs Spain.

Ndimi Luqman MALOTO
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad