Mahakama kuu ya jijini Abuja imeivunja rasmi ndoa ya Paul Okoye wa P Square



August mwaka jana, Anita alikimbilia mahakamani kudai talaka kwa maelezo kuwa ndoa imekuwa karaha kwake na kukosa furaha huku akitaja kuwa amekuwa akisalitiwa na mumewe huyo, walishaanza kutengana, alikuwa baba asiyewajibika vizuri huku pia akidai kutapeliwa naira milioni 10(Tsh.52 million) na Paul Okoye ambazo yeye Anita alizitoa kwa makubaliano ya kufanya biashara ya kampuni aliyoianzisha lakini mumewe alijifanya kujenga ofisi waliyokubaliana lakini ikawa ofisi hewa

Hata hivyo, Anita ambaye alishiriki vikao vya mahakama kwa njia ya Zoom akiwa Marekani anakoishi sasa na watoto wao 3, baadaye alishindwa kuthibitisha madai yake moja kwa moja ikabidi tu wafanye makubaliano ya kuachana Kama wazazi ila mahakama imeitengua rasmi ndoa yao na kuwapa wote uangalizi wa watoto waliozaa

Kwa upande wa Paul Okoye tayari kwasasa ana mahusiano na mwanamke mwingine ambaye amemuweka wazi huku Anita akiendelea na maisha yake Marekani anakoishi na watoto watatu waliozaa pamoja

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad