Makocha wa5 bora Kombe la Dunia



FAINALI za Kombe la Dunia la FIFA za 2022, zilianza Jumapili ya Novemba 20, mwaka huu na Ecuador iliwafunga wenyeji, Qatar 2-0 katika mechi ya ufunguzi. Timu 32 zinapambana ili kunyakua zawadi kubwa zaidi ya mchezo huo mwezi ujao.

Mashabiki wa soka wanasubiri kwa hamu kuona wachezaji bora katika mchezo wakiingia vitani. Lakini nafasi ya timu yoyote kuwa na mbio nzuri kwenye mashindano, itaamuliwa sana na akili za busara zinazofanya kazi pembeni.

Ndio maana umuhimu wa makocha katika mashindano kama Kombe la Dunia hauwezi kupuuzwa. Hapa tunawaangalia makocha bora kwenye Kombe la Dunia la FIFA la 2022.

#5. Didier Deschamps (Ufaransa)

Didier Deschamps aliiongoza Ufaransa kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 2018. Mchezaji huyo wa zamani wa Ufaransa, amefanya kazi nzuri sana akiwa kocha wa 'Les Bleus' hao, na kuiongoza timu hiyo kushinda mara 84 katika mechi 132. Ana kiwango cha ushindi cha asilimia 63.64.

Deschamps pia aliiongoza timu ya Ufaransa kwa ushindi wa 2020-2021 kwenye Ligi ya Mataifa ya Uefa. Kwa urahisi ni mmoja wa makocha waliofanikiwa zaidi kwenye Kombe la Dunia la FIFA la 2022.


Hata hivyo, Deschamps anakabiliwa na kibarua kigumu cha kukiongoza kikosi chake kutetea ubingwa kwa mafanikio wakati huu. Ufaransa si kikosi chenye nguvu kama ilivyokuwa miaka minne iliyopita. Wamefanikiwa kupata ushindi mmoja pekee katika mechi zao sita zilizopita kwenye mashindano yote kabla ya Kombe la Dunia.

#4. Lionel Scaloni (Argentina)

Argentina ni moja ya timu zinazoangaliwa sana kwenye Kombe la Dunia na hiyo inatokana na ukweli kwamba hii inaweza kuwa michuano ya mwisho kwa Lionel Messi. Lakini pia kuna sababu nyingine za mashabiki wa Argentina kushangilia.

Argentina waliingia kwenye michuano hiyo wakiwa hawajafungwa katika mechi 36 kabla ya Saudi Arabia kuivunja rekodi hiyo kwa kuwachapa 2-1 na pia wana kikosi kilichojaa nyota wengi. Kocha wao Lionel Scaloni alikuwa bidhaa isiyojulikana sana katika duru za kimataifa, lakini kwa hakika amethibitisha thamani yake katika miaka michache iliyopita.


Scaloni aliwaongoza 'La Albiceleste' hao kutwaa ubingwa wa Copa America mwaka 2021 na kumaliza ukame wa miaka 28 katika mashindano hayo. Timu ya Scaloni ya Argentina imeshinda michezo 33 kati ya 48 katika mashindano yote hadi sasa kabla ya Kombe la Dunia.

#3. Tite (Brazil)

Brazil inatazamwa na watu wengi kama wenye nafasi kubwa zaidi kutwaa kombe hili mwaka huu. Wana moja ya kikosi bora kwenye mzunguko wa kimataifa hivi sasa na wachezaji wao wengi wako katika hali nzuri. Tite pia aliiongoza Brazil kunyakua taji la Copa America 2019 na amefanya kazi nzuri na timu hiyo katika miaka ya hivi karibuni.

Mwanafunzi huyo nguli Luiz Felipe Scolari, Tite ameifanya Brazil kuwa timu namba moja duniani kwa viwango vya FIFA. Rekodi ya Tite inajieleza yenyewe. Chini ya ukufunzi wake, Brazil wameshinda mechi 57 kati ya 76 katika mashindano yote na kocha huyo wa Brazil ana kiwango cha ushindi cha asilimia 75.

#2. Luis Enrique (Hispania)

Luis Enrique ni mmoja wa makocha bora na wenye uzoefu zaidi katika Kombe la Dunia. Enrique alipata mafanikio mengi akiwa na Barcelona kati ya 2014 na 2017 kabla ya kuchukua nafasi ya ukocha mkuu wa 'La Roja' hao.


Enrique bila shaka ndiye mtu anayefaa kuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Hispania. Kutokana na  kipindi chao cha mafanikio zaidi katika soka la kimataifa, Hispania ilidorora baada ya ushindi wao wa Euro 2012.

Lakini Enrique anaonekana kufufua kikosi hicho, na hadi sasa ameiongoza timu hiyo ya Hispania kushinda mara 19 katika mechi 35. Chini ya uongozi wake, Hispania wamepoteza mechi nne pekee katika mashindano yote.

Anatumaini kwamba kwa kuzungumza moja kwa moja na mashabiki, ataweza kuwapa maarifa ambayo hapo awali yalitolewa kwa vyombo vya habari pekee.

#1. Hans-Dieter Flick (Ujerumani)

Hans-Dieter Flick alithibitisha sifa zake za ukocha kwa ushindi wa kihistoria na Bayern Munich katika msimu wa 2019-20. Baada ya miaka miwili ya mafanikio makubwa kama kocha mkuu wa Bavaria hao, Flick alichukua jukumu la kuinoa Timu ya Taifa ya Ujerumani.


Kombe la Dunia la FIFA la 2022 ni michuano ya kwanza ya kimataifa wa Flick mbali na Ligi ya Mataifa ya UEFA. Ujerumani imekuwa timu ya kutisha chini ya kocha wao mpya, ikishinda 10 na kupoteza mara moja tu katika mechi 16 za mashindano yote hadi sasa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad