“Mama Nimekuelewa Kuhusu Mabehewa” Kigwangalla



Mbunge wa Nzega Vijijini, Hamis Kigwangalla @hamisi_kigwangalla amesema anaunga mkono Serikali kukopa fedha nje ili kuwekeza fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ya kimkakati kama ujenzi wa Reli a Bandari

“Kukopa ni lazima ili pesa za ndani tuzitumie kujenga madarasa, barabara, vituo vya afya na zahanati vijijini, na kulipa mishahara na madeni yetu ya zamani”

“Mradi wa kutanua Bandari ya Dar utaongeza idadi ya vyombo kwa zaidi ya 260%, mradi wa Reli utaongeza tija na ufanisi wa Bandari, hi itaongeza mapato ya kodi, ushuru na tozo mbalimbali”

“Kama Bandari yetu ikiingiza mapato ya 0.5m (crudely) kwenye kila tani, na kama kwa mwaka mmoja tukiwa tunahudumia tani 18m za mzigo, maana yake tunapata mapato ya takribani trilioni 9 kutoka kwenye Bandari tu”

“Tukikopa ili kutanua Bandari na kuienga Reli ya Kisasa kwa haraka, leo badala ya kesho, tuko sawa kabisa, kukoa ill kuwekeza kwenye miradi ya kimkakati inayoenda kuzalisha pesa ina-make sense sana!, hili naliunga mkono”

“Kama mradi wa kutanua Bandari na kununua mashine za kuhudumia mizigo za kisasa bandarini unagharimu trilioni zaidi ya 1, na kama mradi wa SR unagharimu trilioni zaidi ya 16, a kwa kuwa tunaihitaji miradi yote hii leo na siyo kesho, kukopa ina-make sense mno”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad