Marekani na Urusi Wabadilishana Wafungwa


Urusi leo imemuachia huru mchezaji nyota wa mpira wa kikapu kwa wanawake raia wa Marekani Brittney Griner.

Maafisa wa Urusi na Marekani wamesema Griner ameachiwa katika hatua ya ngazi ya juu ya ubadilishanaji wa wafungwa, huku Marekani ikimuachia Viktor Bout, raia wa Urusi anayejihusisha na uuzaji silaha kimagendo.

Ubadilishanaji huo wa wafungwa umefanyika huko Abu Dhabi na umefanyika wakati wa mivutano mikubwa iliyoko kati ya Marekani na Urusi kuhusiana na vita vya Ukraine.

Makubaliano haya ya kubadilishana wafungwa ambayo ni ya pili kufanyika katika kipindi cha miezi 8 kati ya nchi hizi mbili, yamepelekea kuachiwa kwa mtu maarufu zaidi raia wa Marekani aliyekuwa amefungwa nje ya nchi yake.

Rais Joe Biden alizungumza na Griner kwa njia ya simu hapo jana mbele ya mkewe Cherelle, katika ikulu ya White House.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad