Mashabiki wa Diamond Wahoji Kuhusu Afya Yake Baada ya Kulazwa Hospitalini



Diamond Platnumz alipakia picha tofauti na video akionekana kuwa na maumivu akiwa amelazwa hospitalini
Msanii huyo mashuhuri wa nyimbo za Bongo alisema kwamba siku kuu yake ya Krismasi imevurugika baada ya kuugua


Mashabiki wa staa mashuhuri wa Tanzania Diamond Platnumz wameonyesha kuwa na wasiwasi kuhusu hali ya kiafya ya mwimbaji huyo wa Bongo.


Mwanamuziki huyo wa Bongo alipakia video siku kuu ya Krismasi akiwa kwenye kitanda cha hospitali.

Diamond alionekana akiwa na maumivu huku akiwa kwenye mashine mamabyo hupima kiwango cha mpingo wa moyo.


Picha nyingine ilimuonyesha mhudumu wa afya akimshughulikia nyota huyo wa Bongo, huku akiwa amefunga macho kama kwamba alihidsi maumivu.


Kwenye video aliyopakia katika mtandao wake wa Instagram, Diamond alionekana kuwa na 'drip' mkononi mwake.

Msanii huyo wa kibao cha Amaboko alikiri kwamba hajakuwa na siku nzuri na kuandika:

"Bad Christmas this year.”

Mashabiki wake walimtakia uponyaji wa haraka, ila wengine walishangaa iwapo alikuwa akisaka kiki.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad