Mauaji ya Mwandishi Kenya yalipangwa: Ripoti



Ripoti ya timu ya uchunguzi kutoka nchini Pakistan, imesema mauaji ya Mwandishi wa Habari Arshad Sharif (50), yaliyotokea nchini Kenya yalipangwa.


Ripoti hiyo imetolewa ikiwa ni wiki kadhaa baada ya mauaji hayo ya kutatanisha kuzusha shutuma na miito ya kufanywa uchunguzi huru, huku taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi la Kenya ikikinzana na ripoti hiyo ya mauaji hayo.



Nyumba ya milele ya Mwandishi wa Habari Arshad Sharif (50), aliyeuawa nchini Kenya. Picha ya IPI

Aliyeuwa mke na mtoto ahukumiwa kunyongwa

Tayari Polisi Islamabad, imewafungulia mashitaka wafanyabiashara wawili wa Kipakistan wanaoishi Kenya ambao walikuwa ni wenyeji wa mwandishi Arshad Sharif, kwa kuhusika na mauaji yake.


Sharif alikuwa mafichoni nchini Kenya, ili kukwepa kukamatwa nyumbani kwa tuhuma za kudhalilisha taasisi za kitaifa za Pakistan ambapo maafisa wa Pakistan walikwenda Kenya ambako walikutana na Polisi na wenyeji wa Sharif, ambao ni ndugu wawili Kuram na Wagar Ahmed.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad