Maya Mia, Make Up Artist Aliyekuwa Girlfriend wa Idris Sultan, Ommy Dimpoz Afariki Dunia




Make Up Artist Mashuhuri, @maya_mia_y amefariki dunia. Taarifa za kifo chake zilianza kusambaa Jumamosi hii kupitia post za watu wake wa karibu kwenye mitandao ya kijamii.

Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na mamlaka husika, zimedai kuwa kifo chake kimetokana na kujiua kwa kujipiga risasi. Maya ambaye ni raia wa Macedonia, alikuwa akiishi nchini Afrika Kusini alikohamia miaka kadhaa iliyopita baada ya kuishi Tanzania kwa zaidi ya miaka 10.

Alihamia nchini humo baada ya ndoa yake na Mtanzania kuvunjika. Huko aliendelea na kazi yake ya kufanya make up ambayo imempa umaarufu mkubwa duniani.

Maya aliwahi kuwa na uhusiano na Idris Sultan mwaka 2018 kabla ya kuachana na kisha akawa na uhusiano na Ommy Dimpoz kuanzia mwaka 2020 na wameendelea kuwa karibu hadi umauti wake.

Kupitia Insta Story, Ommy ameweka picha akiwa na Maya na kuandika ‘RIP My Love.’ Kwa upande wake Idris Sultan ameweka mkusanyiko wa video na picha enzi wakiwa pamoja na kuandika “Innalillahi wainna illaihi rajighun.”

Maya alikuwa rafiki mkubwa wa Mwamvita Makamba ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 19. Kuomboleza kifo cha rafiki yake, Mwamvita ameweka video kwenye ukurasa wake inayomuonesha Maya akicheza muziki kwenye private jet pamoja na binti wa Mwamvita, Malaika Gray na kuandika “I love you FOREVER Maya Mia.”

Mwingine aliyeomboleza kifo chake ni staa wa Afrika Kusini, @pearlthusi aliyeandika RIP Lovely Lady. May love and many blessing rain upon you as you continue your journey…”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad