Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Msumbiji Luis Jose Miquissone amekubali kurejea Simba SC, ili kuendelea kulinda kiwango chake katika kipindi hiki ambacho ametolewa kwa mkopo akitokea kwa Mabingwa wa zamani wa Afrika Al Ahly.
Miquissone aliuzwa kwa mkopo klabu ya Abha ya Saudi Arabia, kufuatia kiwango chake kutoridhisha tangu aliposajiliwa Al Ahly akitokea Simba SC mwanzoni mwa msimu uliopita.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC Salim Abdallah ‘Tyr Again’ amethibitisha taarifa za Miquissone kuwa tayari kurejea klabuni hapo kupitia dirisha dogo, lakini amesisitiza kuwa hawatoweza kumsajili kutokana na kutakiwa kutoa dau la Shilingi Mililioni 600 kama ada yake ya usajili.
Simba SC yaikaribisha Young Africans mezani
“Dau la Shilingi Milioni 600 ni kubwa kwetu kulitoa kwa mchezaji mmoja na badala yake uongozi umepanga kuachana naye, licha ya yeye mwenyewe kukubali kurejea tena kwetu.”
“Kiasi hicho cha fedha ni kikubwa kama klabu hatuna uwezo wa kumpa na badala yake tutaangalia mchezaji mwingine wa aina yake tutakayemsajili katika Dirisha Dogo.”
“Tunaheshimu kiwango cha Luis. lakini ukubwa wa dau hilo la fedha limetufanya tuachane naye na kuangalia mchezaji mwingine wa aina yake tutakayemsajili.”
“Tunafahamu na kuheshimu kiwango bora cha Luis, lakini kama klabu hatupo tayari kumpatia kiasi hicho cha fedha cha Shilingi Milioni 600.” amesema Try Again
Ahmed Ally: Tutasajili dirisha dogo
Simba SC ilimsajili Luis Miquissone wakati wa Dirisha Dogo msimu wa 2019-20 akitokea nchini kwao Msumbiji alikokuwa akiitumikia Klabu ya UD Songo.
Kiungo huyo alicheza kwa mafanikio makubwa Simba SC akitwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo na kutinga Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu wa 2021-22