Mara nyingi nilikuwa nawaeleza kwamba hili penzi la Wema na Whozu limekaa kibiashara lakini mlikuwa hamuamini.
Hivi sasa Wema na Whozu hawapo pamoja tena, labda Whozu aongeze mkataba wa kiki hiyo ya Mapenzi.
Wema alianza Ku-post Snapchat kwamba anatamani Kufa, watu wakajua tu ameshatibuana na Whozu wala hakuna lingine.
Katika muendelezo huo huo amefuta picha zote za Whozu ambazo amewahi kuzi-post kwenye Page yake. Hii ni dalili tosha kwamba wawili hao hawapo pamoja tena. Mbaya zaidi leo hii Wema ame-post Clip akicheza na Mwanaume Mwingine, Laiti kama angekuwa na Whozu wala asingeweza ku-post.
Tunda na Whozu wamekutana wote chenga sana, Whozu analipia kiki za mapenzi, Huku Tunda analipwa kwa kiki za Mapenzi. Hatari sana.
Kama Kweli Whozu alikuwa anatoka na Wema basi ana gundu, Uhusiano hauna hata Miezi Mitatu ameachika.
By Hopetyga