Morocco amaliza shughuli, Afrika zatangulia mbili 16 bora




TIMU ya Taifa ya Morocco, imekuwa timu ya pili kutoka Afrika kufuzu hatua ya 16 bora, mara baada ya ushindi wa maba0 2-1 dhidi ya Canada katika mchezo wa mwisho wa kundi F, uliopigwa Uwanja wa Al Thumama.

Morocco sasa inakuwa timu ya pili kutoka Afrika, kupita katika hatua hiyo, baada ya Senegal kufanya hivyo. Hii ni mara ya pili kwa Morocco kucheza 16 bora, ikumbukwe aliwahi kufanya hivyo mwaka 1986 nchini Mexico.


Katika mchezo huo, mabao ya Morocco yamefungwa na Hakim Ziyech dakika ya nne, Youssef En Nesyri, dakika 23, bao pekee la Canada limefungwa na Nayef Aguerd aliyejifunga. dakika ya 40.

Matarajio mengine yamebaki kwa Ghana ambaye atamaliza mchezo wake na Uruguay, huku Cameroon bado akiwa na hali ngumu, licha ya kwamba kwenye soka lolote linawezekana.



Mchezo mwingine wa kundi hilo, Belgium imetoa sare ya bila kufungana na Croatia. Katika msimamo wa kundi Morocco ameamliza nafasi ya kwanza akiwa na pointi saba, Croatia nafasi ya pili akiwa na tano, Belgium imebaki na pointi nne na Canada ameondoka akiwa hana pointi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad