Mtoto Kichanga Aliyepotea Siku Saba Apatikana Akiwa Hai


Mtaa wa Migera, Kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera amepatikana akiwa hai mjini Dodoma baada ya kupotea takribani wiki moja.


Mtoto huyo aliibwa Desemba 01, 2022 akiwa amelala kitandani ndani ya nyumba baada ya mama, Johanitha Augustino kuwasindikiza wageni waliokuja kumpa hongera ya kujifungua.

Mama wa mtoto huyo, Johanitha Augustino akiongea na waandishi wa habari amelishukuru jeshi hilo kwa kusaidia upatikanaji wa mwanae na kusema kuwa Desema 8,2022 amepata taarifa ya kupatikana kwa mtoto wake kutoka kwa jeshi la hilo na kumtaka kwenda Dodoma kumfuata mtoto wake.

"Tulifika Dodoma saa 1:30 jioni mtoto alikuwa ameishachukuliwa vipimo na mie wakanichukua vipimo siku iliyofuata majira ya asubuhi wakanikabidhi mtoto na nikaonyeshwa mtuhumiwa, nikarudi Bukoba nikiwa na maaskari polisi" amesema Augustino

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani, Kagera William Mwampaghale akiongea na waandishi wa habari amesema jeshi hilo linawashikilia watu watano ambao hakutaja majina yao wala jinsia zao wanaohusika na wizi wa mtoto huyo.

"Mara baada ya kuripotiwa kwa tukio hilo tulianza uchunguzi mara moja na msako mkali ulifanyika kuanzia Desemba 02,2022 hadi Desemba 08,2022 watuhumiwa hao walianza kukamatwa kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti mkoa wa Kagera na jijini Dodoma" amesema Mwampaghale

Ameeleza kuwa, mtoto huyo baada ya kuibwa alipelekwa kata ya Kamachumu Wilaya ya Muleba kwa mganga wa jadi ili afanyiwe dawa asimsumbue aliyemchukua.

Ameendelea kueleza kwamba, mara baada ya kutoka kwa mganga huyo watuhumiwa hao walitawanyika na mtuhumiwa aliyekuwa amemchukua mtoto alielekea Dar es salaam na wengine walijificha maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa Kagera wakihofia kukamatwa.

"Msako mkali uliendelea ambapo mtuhumiwa aliyekuwa amekimbilia Dar es salaam mara baada ya kugundua anafuatiliwa aliondoka na kwenda kujificha jijini Dodoma na ilipofika Desemba 08, 2022 majira ya saa12:00 jioni mtuhumiwa alikamatwa akiwa na mtoto huyo"Amesema Mwampaghale

Ameongeza kuwa, hali ya kiafya ya mtoto huyo ni nzuri na yupo chini ya uangalizi na watuhumiwa wote wamehojiwa na kukiri kuhusika kwenye tukio hilo, na mama aliyekuwa na mtoto amedai alikuwa na msongo wa mawazo hivyo alimuiba ili amulee, watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya tatatibu za kiupelelezi kukamilika ili sheria ichukue mkondo wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad