Mtoto wa Miaka SITA Ajinyonga kwa Chandarua

 


Simanzi, vilio na huzuni vimetawala katika kijiji cha Ndurumo kata ya Mtapenda Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi, kufuatia mtoto Tumaini Emmanuel (6), ambaye amepoteza maisha baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya chandarua juu ya mti wa mwembe.


Tukio hilo, limethibitishwa kutokea na Jeshi la Polisi Mkoani Katavi, ambapo imearifiwa kuwa Mtoto alijinyonga na kamba iliyokuwa ikining’inia kwenye mti wa Muembe.

Wakizungumza kwa masikitiko, Mama wa Mtoto Juliana Kiyana na baba wa Mtoto, Emanuel Sambilo wamesema tukio hilo limetokea maeneo ya nyumbani kwao kipindi ambacho wao walikuwa katika shughuli za shamba huku wakidai binti yao hakuwa na ugomvi na mtu.


Majirani walliofika na kushuhudia tukio hilo, wamesema wamesikitishwa kutokea tukio hilo huku wakitoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini na maeneo wanayochezea watoto kwa kuhakikiha hakuna vitu vinavyoweza kuhatarisha maisha yao.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ndurumo, Paulo Martini amesema baada ya tukio hilo kutokea walitoa taaraifa kwa jeshi la Polisi na kufanya uchunguzi kisha wakaruhusu taratibu za mazishi zifanyike kwa Mtoto Tumaini Emanueli ambaye ameziowa katika mashamba ya wazazi wake.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad