Mahakama ya Chuka nchini Kenya, imemuhukumu James Kifo Muriuki mwenye umri wa miaka 32 kifungo cha miaka 50 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumnyanyasa kingono mkewe na kuhatarisha maisha yake.
Mnamo tarehe 16 Mei 2020, James alimvuta mkewe hadi mto Kathita na kumtaka abaki utupu Kisha akaanza kunyunyizia pilipili kwenye sehemu zake za siri, chumvi na kuendelea kumfunga kwa gundi aina ya Super Glue.
Hakuishia hapo, James Kifo aliendelea kumziba mkewe mdomo wake na masikio yake kwa Super glue huku mtoto wao akitazama.
Kilio cha mtoto kilifanya majirani kukimbilia eneo la tukio na kumkimbiza hospitali mwanamke huyo, huku Kifo akitokomea kusiko julikana. Kifo anadai kusalitiwa na mkewe kwa Wanaume wengine kipindi mwanaume huyo alipokuwa akifanya kazi jijini Nairobi.
Baada ya tukio hilo, James Kifo alikimbilia kujificha kwa mganga mmoja huko Kitui hadi polisi walipomkamata tarehe 21 Mei 2020.