Mwanamuziki Mwana FA Awashukia Basata Kuhusu Wimbo Mpya wa Dulla Makabila


Baada ya @basata.tanzania kumtaka @dullamakabila kufika kwenye ofisi za Baraza hilo la sanaa nchini ili kujadili kuhusiana na wimbo wake mpya wa PITA HUKU, Mbunge wa Muheza na Rapa #MwanaFA ameandika barua ya wazi akipendekeza kipi BASATA wanapaswa kufanya juu ya Dulla Makabila. Mwana FA ameandika....

“Ni matumaini yangu kikao kilichomuitisha @dullamakabila kwa walezi wetu @basata.tanzania hakitafikia maamuzi ya kukandamiza sanaa kwa kuzuia ubunifu huu mkubwa. Namuaminia Dr Mapana kama msanii mwenzetu na siamini ana nia ya kupiga nyundo sanaa iliyotengenezwa kwa akili nyingi hivi..itakuwa ni kikao kazi flani hivi cha kuelekezana mawili matatu tu na kijana wake Dulla. Pengine hata kumpongeza tu. Hiyo ndio imani yangu. Dude lina maonyo makubwa na kutukumbusha kisanii kabisa kwamba tumejisahau.

Turudi kwenye mada yenyewe. Dude kali sana hili,moja ya singeli ambazo huhitaji kuiskiza mara ya pili ndio ikufikie,SANAA KABISA. Na mtaa umeitikia wito huu. Mambo yote ya humu yapo na yanatakiwa kukemewa kisanaa hivi. PITA HUKU.” Mwana FA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad