Mwanasheria wa Yanga Anyoosha Maelezo Sakata la Fei Toto "Kilichofanyika ni Uhuni Fei Bado ni Mchezaji wa Yanga"




@simon.esq ameweza kunyoosha maelezo juu ya Tetesi za Feitoto kuondoka Klabu ya Yanga na Kujiunga na Azam FC.

Kupitia Instagram ameandika....

"Nimepigiwa simu nyingi mno kila mtu akitaka kujua sintofahamu ya mchezaji wetu “Fei Toto”, kwa kuwa nipo likizo sitaweza kujibu kila mtu bali nitasema yafuatayo;

1. Mikataba ya wachezaji ni standard ya fifa na vipengele vyake vyote ni kwa mujibu wa sheria ya fifa “Regulations on the status and transfer of players”, mikataba hii imeanza kutumita toka mwaka 2002 kufuatia migogoro kadhaa ya wachezaji na vilabu.

2. Kila mkataba ili utambulike na FIFA lazima uwe na kipengele cha kuvunja mkataba husika, mazingira ya kuvunja mkataba yameainishwa wazi kabisa (Article 15 - FIFA regulations on the status and transfer of players) - existance of just cause reason.

3. Kama hakuna “just cause reason” mchezaji anaweza kuondoka kwa njia ya uhamisho tu, na masharti ya uhamisho yapo kwenye kipengele cha 18 cha mkataba wa Fei Toto.

4. Kuna tofauti kati ya kuvunja mkataba na kununua mkataba, kuvunja mkataba lazima sababu zilizoainishwa na FiFA ziwepo, kununua mkataba ni kulipa hela ya release clause.

5. Je Fei Toto anaweza kununua mkataba wake na kuondoka? Jibu ni Ndiyo, sheria ya FiFA inaruhusu mchezaji kununua mkataba wake kwa kuzingatia release clause, na kipengele hicho kipo wazi kwenye mkataba wa Fei Toto kipengele cha 18 na gharama yake iko wazi. Kilichofanyika ni uhuni tu, Fei ni mchezaji halali wa Yanga

NB: Nawaomba Wanayanga tusihamishe focus kwenye mchezo wetu wa jumapili, alama 3 za Azam Fc ni muhimu sana.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad