Ommy Dimpoz Aibiwa Milioni 31 Huku Akiomboleza Kifo cha Mpenzi Wake


Nyota wa Bongo Fleva, mwimbaji @ommydimpoz ambaye kwa sasa anaomboleza kifo cha aliyekuwa mpenzi wake, Maya Mia (Make Up Artist Mashuhuri) raia wa Macedonia aliyefariki dunia mwishoni mwa wikiendi iliyoisha, ametoa taarifa kuwa ameibiwa kiasi cha Shilingi Milioni 30.

Dimpoz amebainisha hilo kupitia insta story yake ambapo ameeleza, siku ya jana ameibiwa kiasi hicho cha fedha ($13K), ambazo ni sawa na takribani Tsh. Milioni 30+ huku akiongeza kuwa ameamua kumshtakia Mungu kwa aliyetekeleza wizi huo.

"Yani hata sijapoa na msiba, jana nimeibiwa Dola elfu 13, almost Milioni 30 hiyo lakini nimeamua kumshtakia Allah🙏" - @ommydimpoz

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad