Ozil amtetea vikali Ronaldo dhidi ya kejeli za vyombo vya habari na wachambuzi wa soka



Aliyekuwa kiungo na mkali wa asisti wa timu za Real Madrid na Arsenal Mezut Ozil amejitokeza kumtetea Staa wa Ureno Christiano Ronaldo dhidi ya kashfa kutoka kwa baadhi ya makundi.

Ozil ambaye walicheza na Ronaldo kwa misimu kadhaa katika timu ya Real Madrid alisuta baadhi ya vyombo vya habari na wachambuzi wa soka wanaomkejeli Ronaldo kuwa ndiye nuzo dhaifu katika timu ya taifa ya Ureno huko Qatar ambapo mashindan ya kombe a dunia yanaendela.


“Sielewi ni wapi uzembe huu wa mara kwa mara kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu Cristiano unatoka ... Vyombo vya habari vinajaribu tu kupata mibofyo, na wadadisi ambao hawana taaluma tena wanataka tu kupata umaarufu na jina lake kuu na kujaribu kumfanya aonekane mbaya,” Ozil aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Aliwataka wakosoaji wa taaluma ya soka ya Ronaldo kukoma na kumpisha kwani tayari ameonesha weledi wake wa viwango vya juu katika soka kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Ozil alisema kuwa wengi wa wanaomkejeli na kumponda Ronaldo hata hawawezi kufikia rekodi zile ambazo amevunja na kuandikisha. Alisema badala ya kumponda, wanafaa kumsherehekea kama nguli wa muda wote katika malimwengu ya soka ambaye hatawahi tokea mtu mwingine kama yeye.

“Hivi karibuni anafikisha umri wa miaka 38 - kwa hivyo ni mshangao gani kwamba hafungi tena mabao 50 kwa msimu? Kila shabiki wa soka huko nje anapaswa kufurahi kumuona akicheza soka la kiwango cha dunia kwa miaka 20 - sidhani kama kuna mtu yeyote kutoka kizazi kipya ataweza kufikia namba zake tena. Atakuwa katika jamii yake milele. 🐐 Kila mtu anapaswa kuonyesha heshima zaidi kwa mmoja wa wanariadha wakubwa katika historia ya michezo...” Ozil alisema.

Zogo la Ronaldo zimekuwa likienezwa kuwa kuna damu mbaya baina yake na baadhi ya watu katika kambi ya timu ya Ureno huko Qatar, haswa baada ya kuwekwa kwenye benchi katika mechi dhidi ya Uswizi ambayo walishinda mabao 6-1 na kufuzu robo fainali.

Ureno inatarajiwa kushuka dimbani Jumamosi kumenyana na Morocco katika mechi ya kufuzu nusu fainali na haijulikani kama nyota huyo wa Ureno ataanzishwa kwenye kikosi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad