SITAKI! Mlimbwende matata mitandaoni (socialite) wa Bongo, Jacqueline Obeid ‘Posh Queen’ @poshyqueeen ambaye anatengeneza vichwa vya habari mitandaoni baada ya kuwa ni msichana mwenye umbo kali aliyemaliza Stashahada ya Insurance and Risk Management katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) cha jijini Dar, amesema hataki kuajiriwa kwani anajua atakavyosumbuliwa.
Posh aliiambia Over Ze Weekend kuwa, anamshukuru Mungu kwani hata alipokuwa chuoni alikuwa ameshaanza kufanya biashara hivyo baada ya kumaliza chuo atajiari mwenyewe. “Sitaki kuajiriwa maana najua nitakayokutana nayo. Ni bora kujiajiri mwenyewe nitakuwa huru na umbo langu,” alisema Posh mwenye mzigo wa maana nyuma.