Rais wa Yanga “Hakuna Mchezaji Ataondoka Yanga”



Rais wa Yanga SC Hersi Said leo amefanya mahojiano maalum na Azam TV na kuwatoa hofu wana Yanga SC kuwa hakuna mchezaji muhimu atakayeondoka Yanga SC kwa sasa.

Hersi amefika mbali na kueleza kuwa hata Feisal Salum hawezi kuondoka sababu bado ana msimu mmoja na nusu hadi 2024 lakini kingine hawezi kuondoka mchezaji yoyote sababu ya wana negotiations power (Nguvu katika mapatano).

“Kama club kwanza nataka niwahakikishie hakuna mchezaji mzuri ataondoka Yanga, tufute kwenye akili zetu hakuna mchezaji ataondoka Yanga katika utawala wetu ambaye sisi tunamuhitaji abaki” >>> Hersi

“Feisal mkataba wake unaisha 2024 bado yupo sana ana msimu huu ana msimu ujao halafu Feisal ni moja kati ya wachezaji muhimu kwenye kikosi chetu” >>> Hersi VIA Azam TV

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad