Napenda kuona vijana wakionesha uwezo wao, vijana walipwe kwa kadri ya wanachokionesha, wapate thamani kwa kadri ya wanachokionesha uwanjani, mwisho wa siku ni maisha na bado nguvu ipo wanapaswa kuvuna kupitia soka.
Mpira wa mahaba, mapenzi na hisia umepitwa na wakati, kila mkikutana mezani ni dili jipya kwa pande zote mbili, timu inakutumia na wewe wa leo sio wa kesho, ni vitu vya muda tu, tambua thamani na iishi thamani.
Ni maisha haya.