Kwa Feisal kutaka kuondoka Yanga kwenda Azam ni kuuwa mpira wake lakini ni sahihi kimaslahi, nadhani Menejimenti yake ingekuwa ina mlengo mzuri wangepaswa kufikiria nje ya nchi sioni sababu abaki tena Tanzania kama sio Yanga.
Nilikuwa Qatar nilipata nafasi ya kuwapa link na Viongozi wake kuna klabu kubwa inahitaji huduma yake, kwangu sio lazima awe kwenye Menejimenti yangu bali ilipopatikana fursa nikaona niwape link.
Ni Mchezaji mzuri ana profile kubwa kama anaondoka Yanga sio kubaki hapa ndani, Azam sio sahihi kwake, nitajie Mchezaji gani aliyefanikiwa baada ya kuhamia Azam.