Shafih Dauda "Ni Kweli Fei Toto Kawalipa Yanga Lakini Amekosea Kwa Mujibu wa Sheria"


Ni kweli Feisal Salum alilipa pesa za kuvunja mkataba wake na Yanga kama nilivyoripoti jana ila baada ya kupitia vifungu vya kisheria na nondo kadhaa kutoka kwa Watalaam wa sheria ni wazi kuwa Feisal AMEKOSEA, hajatumia njia sahihi ya kuondoka Yanga.

Hayupo sahihi kisheria na kiutaratibu, ukisoma 18.1 kuhusu kuondoka wameweka wazi kwenye mkataba ambapo Feisal hajafuata hata kifungu kimoja, ukipitia kuhusu Contract Termination as per FIFA bado Feisal amekwama.

Ni kama amebreach contract na sio kuuvunja kwakuwa utaratibu upo wazi, kilichopo naamini Yanga na Azam watatumia busara, Azam wanamtaka nadhani wafike ofisi za Yanga wamalizane kwakuwa naamini ni sahihi kijana kucheza ila kwa kufuata utaratibu.

Busara itumike japo kijana amekosea lakini room iwepo ili mmalizane vyema na maisha yaendelee.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad