Mahakama ya Sheria katika jimbo la Kano, kaskazini mwa Nigeria, imemhukumu kifo mhubiri mashuhuri wa Kiislamu kwa kumnyonga, baada ya kumkuta na hatia ya kumkufuru mtume Muhammad pamoja na uchochezi katika baadhi ya mahubiri yake.
Sheikh Abduljabar Nasir Kabara anashikiliwa na mamlaka tangu Julai mwaka jana baada ya kutuhumiwa kueneza maubili ya uongo dhidi ya Mtume.
Kesi hiyo inafuatiliwa kwa karibu na Wanigeria.
Kano ni miongoni mwa majimbo 12 kaskazini mwa Nigeria ambapo Sharia inatekelezwa pamoja na sheria za kilimwengu za nchi hiyo. Mwanazuoni huyo mwenye umri wa miaka 52 anatoka katika madhehebu ya Qadiriyya.
Ana idadi kubwa ya wafuasi hasa katika jimbo la Kano. Baba yake alikuwa kiongozi wa dhehebu hilo huko Afrika Magharibi hadi kifo chake mnamo 1996.
Sheikh Abduljabar ana haki ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Hukumu za kifo nchini Nigeria hutekelezwa kwa nadra hivyo watu waliohukumiwa kifo huwekwa magerezani kwa muda usiojulikana