Mwimbaji Mkongwe wa Congo Élisabeth Tshala Muana Muidikay maarufu Tshala Muana amefariki dunia leo December 10 2022, familia imethibitisha.
Mitandao mbalimbali ya Congo imesema Mkongwe huyu amefariki akiwa na umri wa miaka 64 ambapo hata hivyo taarifa iliyotolewa na Familia kupitia facebook haijasema chanzo cha kifo hicho.
Miongoni mwa wanaomlilia Tshala Mwana ni Mkongwe Koffi Olomide na Fally Ipupa ambapo moja ya nyimbo za Tshala zilizopata umaarufu hadi Tanzania ni wimbo wa "karibu yangu" uliokua ukiimba "uniurumie rumie, nakulilia unite, unipeleke kwa mama atatupatia mali tuunge oh ndoa ya lote"