Mfaransa Theo Hernandez akishangilia baada ya kufunga bao lake la kwanza akiwa na Olivier Giroud . katika mechi ya Ufaransa dhidi ya Morocco uwanja wa AlBayt. REUTERS/Dylan Martinez.
Mfaransa Theo Hernandez akishangilia baada ya kufunga bao lake la kwanza akiwa na Olivier Giroud . katika mechi ya Ufaransa dhidi ya Morocco uwanja wa AlBayt. REUTERS/Dylan Martinez.
Timu ya taifa ya Ufaransa Le Bleu imefanikiwa kuingia katka fainali yta kombe la dunia kwa mara nyingine tena baada ya kuifunga timu ya Morocco bao 2-0 katika uwanja wa Al Bayt Doha Qatar.
Alikuwa ni mchezaji Theo Hernandez aliyepachika bao la kwanza katika dakika ya 5 ya mchezo huo na kuwafanya Morocco kuwa nyuma mapema kabisa katika mchezo huo naye mshambuliaji Randal Kolo Muani alipachika bao la pili na kufunga kitabu cha magoli katika dakika ya 79 ya mchezo na kufuta matumaini ya Morocco kucheza fainali ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza.
Timua ya Ufaransa- Le Bleu ilitiwa moyo kucheza mbele ya Rais wao Emmanuel Macron ambaye alikwenda uwanjani kushuhudia mchezo huo.
Na kwa mara ya kwanza tangu mechi ya kufuzu AFCON dhidi ya Afrika Kusini mwezi Juni, Morocco ilianza kwa kuwa nyuma kwa bao la mapema.
Pamoja na Atlas Lions kutafuta nafasi nyingi, mbinu za Ufaransa za kukabiliana na mashambulizi zilizidi kuwa hatari zaidi. Kombora la Kylian Mbappe katioka dakika ya 35 lilimpita Bounou na kuondolewa nje ya mstari, huku kutoka umbali mrefu Giroud akipiga shuti kali lakini likaenda nje ya lango lisilo na ulinzi katika sekunde zilizofuata.
Morocco waliamka katika dakika za mwisho za mchezo huo na kukosa nafasi za wazi katika dakika ya 75 na 77 ambazo kama wangetumia vyema pengine mambo yangebadilika kwa upande wao.
Hata hivyo Morocco, bado wameweka alama ya juu kwa bara la Afrika na ulimwengu wa Kiarabu, na bado watakuwa na mchezo wa kugombea nafasi ya tatu Jumamosi dhidi ya Croatia.
Kwa upande mwingine, Ufaransa itajaribu kutetea taji lao la Kombe la Dunia na kumaliza ndoto tofauti, huku Leo Messi na Argentina nao wakijaribu kutimiza ndoto ya Messi kuinua kombe la dunia hasa akiwa amekwishatangaza kuwa mchezo wa Jumapili ndio wa mwisho kwa timu yake ya taifa.