Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mwananchi Communication Limited, Bakari Machumu amesema sera ya kampuni hiyo haimkatazi mwandishi wa habari kujihusisha na siasa bali akishaingia huko itamlazimu kutoka kwenye chombo hicho.
"Sera ya kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) haimkatazi mwandishi wa habari kujihusisha na siasa anaruhusiwa. Lakini akishaingia huko anatakiwa kutoka ndani ya chombo cha habari na akipata au akikosa haruhusiwi kurudi tena ndani," amesema Machumu.