Update: Baada ya jirani kutoa ushahidi, kesi ya kifo cha Osinachi imeendelea mahakamani ambapo safari hii mdogo wake Osinachi wa kiume kwa jina la Godwin na yeye amepanda kizimbani kutoa ushahidi
Godwin amesema kiujumla Osinachi alikuwa anaishi kwa hofu, kuteswa kwa na kunyanyaswa na mumewe. Godwin amesema kipindi cha nyuma mama yao alikuwa anaumwa hivyo Osinachi akamuomba mumewe mama yake aje hapo nyumbani ili apate matibabu maana wanaishi mbalimbali
Mume hakupendezwa na suala hilo na alipokuja hapo kuna siku mtoto wao mkubwa kwa bahati mbaya alivunja kikombe chenye maji ambapo alipigwa na baba'ke(mume wa Osinachi) hadi ikawa huruma, Mama Osinachi akamuomba amsamehe mtoto maana watoto wanajifunza kupitia makosa lakini kilichotokea baadaye mama yake alitukanwa na mume wa Osinachi na kuitwa mchawi na majina kibao
Na yeye Odwin kuna siku aliombwa na Osinachi amsaidie kazi fulani jikoni lakini shemeji yake alipokuja alianza kuonesha kisirani cha wazi na kutaka ugomvi mwishowe wote yeye na mama yake walitimuliwa na mume wa Osinachi waondoke hapo nyumbani bila kujali mkwe wake anaumwa amekuja kwa ajili ya matibabu. Walienda kusaidiwa pa kuishi kwa muda na rafiki yake pacha wa Osinachi
Kipindi Osinachi ndio anaumwa mama yake alimwambia Godwin aende akamuone kimetokea nini. Alipofika na kugonga geti muda mrefu mtoto mkubwa alijitokeza, mume wa Osinachi alipouliza ni nani akamjibu ni mjomba Godwin akamjibu mwambie arudi alikotoka
Amesema Osinachi alikuwa anaumwa lakini mume wake alikuwa anawaficha hata Hospitali aliyolazwa, baadaye Osinachi aliombba sana ndugu zake waelezwe alipo, Godwin alipofika hospital alimkuta Osinachi ameshikilia kifua kwa maumivu makali, baada ya dokta kuondoka, Godwin alipotaka kumsogelea ghafla mume wa Osinachi akamzuia Godwin asimsogelee Osinachi kisha kuita walinzi wamtoe Godwin
Pia Gowin anasema kuna wakati shemeji yake anarudiarudia maneno ya kutaka kumpiga dada yake hadi kuna siku alipoanza tena ilibidi amjibu shemeji yake kuwa usije ukajaribu kumpiga tena dada. Na muda mwingi Osinachi yupo tu kimya